Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-TRUMP-UCUNGUZI-HAKI

Trump awasilisha majibu yake kwa mwendesha mashitaka Mueller

Rais wa Marekani Donald Trump ametuma majibu yake ya maandishi kwa maswali aliyohojiwa na mwendesha mashitaka maalum Robert Mueller, anayehusika na uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia katika uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 2016, mwanasheria wa rais wa Marekani, Rudy Giuliani, amesema.

Rais wa Marekani Donald Trump anaendelea kukabiliwa na uchunguzi unaoendeshwa na mwendesha mashitaka maalum Robert Mueller kuhusu madai ya Urusi kuingilia katika uchaguzi wa Marekani.
Rais wa Marekani Donald Trump anaendelea kukabiliwa na uchunguzi unaoendeshwa na mwendesha mashitaka maalum Robert Mueller kuhusu madai ya Urusi kuingilia katika uchaguzi wa Marekani. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump alitangaza wiki iliyopita kuwa amekamilisha kujibu maswali kutoka kwa mwendesha mashitaka Mueller na kwamba amekamilisha kazi hii "kwa urahisi sana".

"Mambo mengi yaliyoulizwa yanazua maswali makubwa ya kikatiba na yanakwenda mbali zaidi ya upeo wa uchunguzi halali," Giuliani amesema katika taarifa.

Kwa upande wa Rudy Giuliani, Donald Trump alitoa "ushirikiano usio wa kawaida" na ni wakati sasa wa"kuhitimisha uchunguzi huu".

Hivi karibuni Giuliani aliliambia shirika la Habari la Reuters kwamba mteja wake atatoa majibu kuhusu uwezekano wa kuhusishwa kati ya maafisa wa kampeni yake ya uchaguzi na viongozi wa Urusi wenye uhusiano wa karibu na ikulu ya na Kremlin.

Wiki iliyopita chanzo kimoja kiliisema kwamba Robert Mueller anataka maelezo zaidi kuhusu mkutano wa mwezi Juni 2016 ambapo walishiriki Donald Trump Jr., mtoto wa Rais Donald Trump, maafisa kadhaa wa timu yake ya kampeni na kundi la watu kutoka Urusi.

Rais wa Marekani anaamini kwamba uchunguzi unaoendeshwa na Robert Mueller tangu mwezi Mei 2017 ni "unalenga kumharibia jina".

Donald Trump, ambaye utawala wake umeendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu kutokana na kesi hiyo tangu kuchukuwa hatamu ya uongoxi wa nchi Januari 2017, anasema kuwa hapkuwa na uingiliano wowote wa Urusi katika uchaguzi wa urais nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.