Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-USALAMA

Kumi na mbili wauawa kwa kupigwa risasi California

Watu kumi na mbili wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu aliyejihami kwa bunduki ambaye pia aliuawa katika makabiliano na vikosi vya usalama katika mji wa kaskazini mwa Los Angeles, nchini Marekani.

Tukio hili la mauaji lilitokea katika baa ya Thousand Oaks, kaskazini mwa Los Angeles, Novemba 7, 2018.
Tukio hili la mauaji lilitokea katika baa ya Thousand Oaks, kaskazini mwa Los Angeles, Novemba 7, 2018. Thomas Gorden/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano usiku katika eneo maarufu la burudani la Borderline Bar and Grill,ambako vijana wengi walikuwa wanatarajia kujielekeza, kwa mujibu wa afisa polisi.

Mkuu wa Kaunti ya Ventura County, Geoff Dean, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa watu kumi na mbili waliuawa kwa kupigwa risasi, ikiwa ni pamoja na afisa wa polisi aliyejaribu kuingilia kati. Mshambuliaji pia aliuawa, ameongeza Geoff Dean, huku akibaini kwamba mshambuliaji huyo hakuhesabiwa miongoni mwa watu waliouawa.

Kwa mujibu wa mashahidi idadi ya watu waliojeruhiwa haijulikani, na tayari wamefikishwa katika hospitali mbalimbali.

Mkuu wa Kaunti ya Ventura County, hakuweza kueleza ikiwa mshambuliaji alipigwa risasi na polisi au alijiua mwenyewe akitumia bunduki yake.

Uraia wa mshambuliaji na sababu za mauaji hayo wavijulikani lakini mashahidi kadhaa ambao walikuwa kwenye sehemu hiyo ya Borderline Bar and Grill walieleza kwamba walimuona "mtu mwenye ndevu nyeusi", akishikilia bunduki mkononi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.