rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani China Donald Trump Xi Jinping

Imechapishwa • Imehaririwa

Bloomberg: Marekani yatishia kuweka ushuru mpya kwa bidhaa kutoka China

media
Vita vya biashara vinaendelea kati ya China na Marekani. REUTERS/Damir Sagolj

Marekani inajiandaa kutangaza ushuru mpya kwa bidhaa zinazosalia kutoka China ifikapo mwanzoni mwa mwezi Desemba ikiwa mazungumzo kati ya Marais Donald Trump na Xi Jinping hayatozaa matunda yoyote, kwa mujibu wa shirika la Habari la Bloomberg likinukuu vyanzo visivyorasmi.


Rais wa Marekani na mwenzake wa China watakutana kando ya mkutano wa G20 huko Buenos Aires mwishoni mwa mwezi Novemba.

Hakuna uamuzi ambao umechukuliwa, lakini maandalizi yanaendelea kuandaa orodha mpya ya ushuru kwa bidhaa kutoka China ikiwa mazungumzo hayatazaa matunda, limeongeza gazeti hilo. Taarifa ambayo haijathibitishwa na serikali ya Marekani.

Chanzo kilio karibu na faili hiyo kimeliambia shirika la Habari la Reuters kwamba hali hiyo inaweza kuwa hivo, kikiongeza bila maelezo zaidi, kwamba "mckato umeanza".

Ushuru huu mpya utahusu bidhaa ambazo hazikutajwa hapo awali kwenye orodha ya didhaa zilizowekewa ushuru, sawa na kiasi cha kutosha cha dola bilioni 257, kulingana na takwimu za mwaka jana, Bloomberg imeongeza.

Trump tayari ameweka ushuru wa dola bilioni 250 kwa bidhaa kutoka China na China ilijibu kwa kuweka ushuru wa dola bilioni 110 kwa bidhaa kutoka Marekani.