Pata taarifa kuu
BRAZILI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Jair Bolsonaro ashinda uchaguzi wa urais Brazil

Mwanasiasa wa mrengo wa kulia Jair Bolsonaro, aliyeshinda mzunguko wa kwanza wa Uchaguzi wa urais nchini Brazil, ameshinda uchaguzi wa urais wa duru ya pili kwa kura asilimia 55. Mgombea mwenza Fernando Haddad wa mrengo wa kushoto na chama cha wafanyakazi amepata asilimia 45.

Jair Bolsonaro, Rio de Janeiro mnamo Oktoba 28, 2018.
Jair Bolsonaro, Rio de Janeiro mnamo Oktoba 28, 2018. REUTERS/Pilar Olivares
Matangazo ya kibiashara

Bolsonaro, Mkuu wa zamani wa jeshi alipigia kampeni akiahidi kumaliza rushwa na kupunguza kasi ya Uhalifu.

Katika hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi alisema kuwa atalinda katiba na demokrasia ya Brazil, huku akitia mbele hatima ya nchi hiyo katika masuala ya uchumi.

Sera ya uchumu ya rais Bolsonaro ni kupunguza serikali kuingilia uchumi.

Bolsonaro amesema kuwa atakabiliana na wanasiasa wala rushwa, alitoa ahadi hiyo katika moja ya kampeni zake , jambo ambalo linazungumzwa na wananchi Wengi waliochoshwa na visa vya Rushwa kutoka kwa wanasiasa wakongwe ambao wamewahi hadi kufungwa kwa ajili ya Rushwa.

Bolsonaro atachukuwa hatamu ya uongozi baada ya kutawazwa tareheJanuari 1, 2019 na hivyo kumrithi mtangulizi wake Michel Temer.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.