Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

FBI yawasaka watu waliotuma vifurushi hatari kwa viongozi

Vyombo vya usalama nchini Marekani vinaendesha msako mkali dhidi ya watu wanaotuhumiwa kutuma vifurushi vinavyodhaniwa kuwa ni milipuko kwa viongozi wa zamani na watu mashuhuri.

Vifurushi vinavyodhaniwa kuwa ni milipuko vilivyotumwa kwa viongozi na watu mashuhuri nchini Marekani. Hapa ni kwenye ofisi ya Posta ya Florida.
Vifurushi vinavyodhaniwa kuwa ni milipuko vilivyotumwa kwa viongozi na watu mashuhuri nchini Marekani. Hapa ni kwenye ofisi ya Posta ya Florida. REUTERS/Zach Fagenson
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi polisi walibaini kifurushi kilichotumwa kwa makamu wa rais wa zamani Joe Biden na muigizaji maarufu wa Hollywood Robert De Niro.

Makamu wa rais Mike Pence amewalaumu watu waliotuma vifurushi kwa marais wa zamani akisema watakaopatikana kuhusika na matukio haya watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Si chini ya vifurushi 10 vilivyogunduliwa wiki hii, lakini hakuna hata kifurushi kimoja kati ya vyote hivyo kiliyoweza kulipuka.

Msemaji wa Ikulu Sarah Sanders amelaani jaribio hilo la mashambulio ya vurugu dhidi ya watu mashuhuri.

"Matukio ya kigaidi hayakubaliki popote na mtu yeyote ambaye atakamatwa kuhusika atachukuliwa sheria, " amesema Sarah Sanders.

Uchunguzi bado unaendelea ili hatua sahihi ziweze kuchukuliwa" Msemaji wa White House amesema.

Kifaa cha aina hiyo kiliwahi kutumwa katika ofisi za CNN mjini New York ambapo iliwalazimu waandishi wa habari kukatisha matangazo mara baada ya kusikia kengele ya moto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.