rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Brazili Jair Bolsonaro

Imechapishwa • Imehaririwa

Brazil: Jair Bolsonaro aongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais

media
Wafuasi wa Jair Bolsonaro wakifurahia kura alizopata kiongozi wao baada ya kutangazwa matokeo ya awali Oktoba 7, 2018 Brasilia. REUTERS/Ueslei Marcelino

Mwanasiasa wa mrengo wa kulia Jair Bolsonaro, ameshinda mzunguko wa kwanza wa Uchaguzi wa urais nchini Brazil. Jair Bolsonaro ambaye amepata 46% atapambana katika duru ya pili ya uchaguzi na mgombea wa Chama cha Wafanyakazi, Fernando Haddad, ambaye amepata 29% ya kura.


Bolsonaro, ambaye amepata ushindi wa asilimia 46, atapambana na mgonbea wa chama cha Wafanyikazi Fernando Haddad, aliyepata asilimia 29.

Uchaguzi huu umekwenda katika mzunguko wa pili baada ya mshindi kushindwa kupata asilimia 50 ya kura zote, kama inavyohitajika na katiba ya nchi hiyo.

Jair Bolsonaro (kushoto) na Fernando Haddad (kulia) wanatarajia kupambana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais Brazil. REUTERS/Paulo Whitaker/Nacho Doce

Bolsonaro, amesema kama kusinhekuwa na changamoto katika mfumo wa upigaji kura kwa njia ya kieletroniki, angepata ushindi wa moja kwa moja.

Mzunguko wa pili utafanyika tarehe 28 mwezi huu wa Oktoba, na matokeo haya yamethibitisha kura za maoani kuelekea Uchaguzi huu ambazo zilieleza kuwa hakuna atakayeshinda katika mzunguko wa kwanza.

Fernando Haddad, akizungukwa na wafuasi wake, huko Sao Paulo, Oktoba 7, 2018. REUTERS/Paulo Whitaker