Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA-HAKI

Donald Trump aendelea kumuunga mkono Brett Kavanaugh

Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kumuunga mkono mteule wake katika nafasi ya jaji wa mahakama ya juu nchini humo Brett Kavanaugh, licha ya mteule huyo kujitetea dhidi ya tuhuma za udhalilishaji dhidi ya mwalimu wa chuo kikuu Christine Ford.

Rais wa Marekani Donald Trump akiwa pamoja na Brett Kavanaugh (kushoto).
Rais wa Marekani Donald Trump akiwa pamoja na Brett Kavanaugh (kushoto). REUTERS/Jim Bourg
Matangazo ya kibiashara

Rais Trump amesema haya punde baada ya wabunge wa Seneti kumaliza kuwahoji Kavanaugh na Christine kwa nyakati tofauti, mahoajiano ambayo yalilenga kupata ukweli kuhusu tuhuma za Christine dhidi ya Kavanaugh.

Awali akihojiwa na kamati ya sheria, Christine Ford alieleza namna jaji Kavanaugh alijaribu kumvua nguo wakati wakiwa sekondari katika miaka ya 1980, akiwaeleza wabunge kuwa alihofu kuwa Kavanaugh angembaka.

Christine Blasey Ford, ambaye anayemshtumu Brett Kavanaugh kumdhalilisha, ankitoa ushuhuda mbele ya Bunge la Seneti Septemba 27, 2018.
Christine Blasey Ford, ambaye anayemshtumu Brett Kavanaugh kumdhalilisha, ankitoa ushuhuda mbele ya Bunge la Seneti Septemba 27, 2018. Saul Loeb/Pool via REUTERS

Ilipofika zamu ya jaji Kavanaugh kuhojiwa na kamati hiyo, alikanusha madai dhidi yake katika utetezi ambao wakati wote alikuwa akijibizana na wabunge wa Democrats waliomtaka akubali kuchunguzwa na shirika la upepelezi la FBI, pendekezo ambalo chama cha Republican kinapinga.

Wabunge hao wanatarajiwa kupiga kura baadae hivi leo Ijumaa kumuidhinisha mteule wa rais Trump au la, kura ambayo huenda ikatoa mustakabali wa namna muundo wa mahakama ya juu utakavyokuwa ikiwa Kavanaugh atapitishwa.

Wabunge 51 wa Republican kati ya wabunge 49 wa Democrats ndio watakaoamua hatma ya sakata ambalo limetikisia nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.