Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI

Ripoti: Korea Kaskazini inaendeleza mradi wa kutengeneza makombora

Ripoti zinaeleza kuwa, Korea Kaskazini inaendelea inatengeneza makombora ya masafa marefu licha ya mazungumzo ya mwezi Juni kati ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un na rais wa Marekani Donald Trump.

Makombora ya mbali
Makombora ya mbali Reuters
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa Marekani ambao hawakutaka kufahamika, wameliambia Gazeti l Marekani la Washington Post kuwa, utengenezaji wa makombora hayo unaendelea.

Hata hivyo, haijafahamika ni katika hatua gani mradi huo umefikia.

Wakati wa mkutano wa kihstoria kati ya rais Trump na Kim Jong Un nchini Singapore, Korea Kaskazini  ilitangaza kuwa ilikuwa inasitisha kabisa mradi wake wa nyuklia.

Rais Trump, amekuwa akishtumiwa nyumbani kwa kumwamini kiongozi wa Korea Kaskazini mapema bila ya kujiridhisha kuhusu mradi huo.

Hata hivyo, rais Trump amekuwa akisema kuwa, anamwamini kiongozi wa Korea Kaskazini kuhusu ahadi alizotia na tayari imeharibu maeneo yake ya kujaribu silaha zake.

Wiki iliyopita, Korea Kaskazini ilirejesha mabaki ya Wamarekani waliouawa katika taifa hilo miaka zaidi ya 60 iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.