Pata taarifa kuu
MAREKANI-USURI-USHIRIKIANO

White House: Tutahakikisha Urusi haiingilii tena uchaguzi wa Marekani

Ikulu ya Marekani imesisitiza kuwa Urusi bado ni nchi hatari kwa Marekani. Ni kauli inayokuja wakati huu rais Donald Trump anapoendelea kushtumimiwa kwa matamshi yake wiki hii kuwa anaamini Urusi haikuingilia Uchaguzi wa mwaka 2016, na baadaye kusema kuwa hakueleweka vema.

Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, Julai 16,  2018 huko Helsinki.
Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, Julai 16, 2018 huko Helsinki. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ikulu Sarah Sanders amesema, Marekani inaendelea kufanya bidii kuhakikisha kuwa, Urusi haingilii Uchaguzi wa nchi hiyo kama ilivyofanya katika miaka iliyopita.

Mapema wiki hii Rais wa Marekani Donald Trump aliitetea Urusi, na kusema haikuingilia kwa namna yoyote ile Uchaguzi wa urais mwaka 2016 na kumsaidia kupata ushindi.

Kuali ya Trump, inatofautiana na taarifa ya maafisa wa Inteljensia wa Marekani ambao wameendelea kusisitiza kuwa, Urusi iliingilia Uchaguzi huo.

Trump ambaye alikutana na rais Putin jijini Helsinki nchini Finland, amesema anaamini Urusi haikuwa na sababu yoyote ya kuingilia Uchaguzi huo.

Wakuu wa chama cha Trump wakiongozwa na Spika wa bunge la Congress Paul Ryan, wamekosoa kauli ya Trump huku Seneta John MacCain akisema Trump alitoa kauli za aibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.