rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nicaragua Daniel Ortega

Imechapishwa • Imehaririwa

Jeshi ladai kudhibiti ngome kuu ya upinzani Nicaragua

media
Kikosi maalumu cha Nicaragua kikipiga doria katika mtaa wa Masaya, Julai 17, 2018. ©REUTERS/Oswaldo Rivas

Wanajeshi wa serikali nchini Nicaragua, wamethibiti ngome kuu ya upinzani, katika eneo la Masaya Kuisni mwa jiji kuu, wakati ambapo watu zaidi ya 270 wameuawa katika machafuko yanayoendelea nchini humo kwa mujibu wa mashahidi.


Vikosi hivyo vinavyomuunga mkono rais Daniel Ortega vimekuwa vikipambana na wanaharakti wa upinzani wanaomtaka rais huyo kuondoka madarakani.

Wanaharakati wanasema, watu kadhaa wamepoteza maisha katika makabiliano hayo lakini idadi haiwekwa wazi.

Hata hivyo, serikali imekuwa ikisema mzozo huu wa miezi mitatu umesababisha vifo vya watu zaidi ya 280.

wakati huo Maaskofu wa Costa Rica wanaitaka Jumuiya ya Kimataifa kujihusisha kwa karibu zaidi na machafuko ya kisiasa nchini Nicaragua, ili kuweza kupata suluhu ya kudumu vinginevyo kuna hatari kwa nchi kutumbukia katika maafa makubwa.

Naye Rais Daniel Ortega wa Nicaragua amesema, hana sababu msingi za kuitisha uchaguzi mkuu kwa wakati huu kama njia ya kudhibiti machafuko ya kisiasa nchini mwake. Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama inatoa: kanuni, sheria na taratibu ambazo zinapaswa kufuatwa na Serikali  katika masuala ya uchaguzi mkuu. Hili ni ombi ambali lilikuwa limetolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Nicaragua na kuungwa mkono pia na vyama vya upinzani nchini humo.

Itakumbukwa kwamba, hivi karibuni, Papa Francis aliungana na Baraza la Maaskofu Katoliki Nicaragua ili kuonesha masikitiko yake kutokana na machafuko pamoja na ghasia zinazoendelea nchini humo, ambazo tayari zimepelekea watu kadhaa kupoteza maisha yao na wengine wengi kujeruhiwa vibaya. Kikundi cha watu wenye silaha kinachounga mkono serikali iliyoko madarakani kimeamua kuanzisha mashambulizi ya silaha ili kupambana na raia wanaopinga mchakato wa mageuzi unaofanywa na serikali ya Nicaragua.