Pata taarifa kuu
GUATEMALA-MAREKANI-WAHAMIAJI-USALAMA-HAKI

Guatemala yaomba Marekani kuwapokea raia wake kwa muda

Serikali ya Guatemala imeiomba Marekani kuwapa hifadhi ya muda mfupi wahamiaji wa Guatemala ambao waliyatoroka makaazi yao kufuatia mlipuko wa volkano ya Fuego.

Mlipuko wa volkano ya Fuego,uliuawa watu zaidi ya 100, na kulazimu raia wengi wa Guatemala waliokua wakiishi karibu na eneo hilo kuyatoroka makaazi yao, Juni 4, 2018.
Mlipuko wa volkano ya Fuego,uliuawa watu zaidi ya 100, na kulazimu raia wengi wa Guatemala waliokua wakiishi karibu na eneo hilo kuyatoroka makaazi yao, Juni 4, 2018. REUTERS/Jose Cabezas
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Guatemala Jimmy Morales ametangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba amemuomba waziri wake wa mambo ya Nje kuiomba Marekani kuwapa hifadhi kwa muda raia wake waliolazimika kuhama makaazi yao.

Volkano hiyo, inayopatikana kilomita 40 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Guatemala City, karibu na mji wa ukoloni wa Antigua, ilianza kulipuka tarehe 3 Juni na kuua watu 112. Watu wengi walihamishwa.

Ombi hilo la serikali ya Guatemala linakuja siku mbili baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutoa wito wa kuharakishwa kwa shughuli ya kuwatimua wahamiaji haramu nchini humo bila hata kufuata utaratibu wa mahakama.

Katika ukurasa wake wa Twitter Donald Trump aliandika: "mtu anapoingia ndani, ni lazima mara moja, bila majaji na kesi mahakamani, tuwarejeshe walikotoka."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.