Pata taarifa kuu
COLOMBIA-UCHAGUZI

Ivan Duque ashinda uchaguzi wa urais Colombia

Wapiga kura nchini Colombia wamepiga kura na kumchagua Ivan Duque kama rais wa nchi hiyo. Mgombea kutoka mrengo wa kulia ameshinda na asilimia 54 ya kura dhidi ya Gustavo Petro, mgombea wa mrengo wa kushoto ambaye amekubali kushindwa.

Ivan Duque karibu na mke wake, Juni 17, 2018, mbele ya wafuasi wake baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa rais.
Ivan Duque karibu na mke wake, Juni 17, 2018, mbele ya wafuasi wake baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa rais. REUTERS/Andres Stapff
Matangazo ya kibiashara

Duque anayeungwa mkono na rais wa zamani Alvaro Uribe, amesema kuwa atafanyia marekebisho makubaliano yam waka 2016 ambao uliwapatia waasi wa nafasi ndani ya Congress.

Tangu Jumapili hii, Juni 17, Bw Duque amekua rais mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya sasa ya Colombia. Ivan Duque, 41, amewahutubia wafuasi wake mjini Bogota. Ameahidi kufanyia marekebisho mkataba wa amani uliyofikiwa kati ya serikali na wapiganaji wa FARC.

"Niliamini kabisa kama nitashinda uchaguzi huu ... Nimekua nikikaribiana kabisa na mgombea wa mrengo wa kushoto! Mapambano yanaendelea na historia ya nchi itabadilika, " amesema Bw Duque.

Licha ya kushindwa, wafuasi wa Petro wanataka kuamini kwa mabadiliko.

Mgombea wa chama cha Democratic Centre (DC), ameshinda kwa 54% ya kura dhidi ya 41.8% aliyepata Gustavo Petro, 58, mgombea wa kwanza kutoka mrengo wa kushoto ambaye amepata hadi sasa kura nyingi ikilinganishwa na zile walizopata watangulizi wake katika uchaguzi wa urais. Kwa kura zaidi ya milioni 8 alizopata, Petro sasa anaongoza upinzani.

Bwana Duque anatajwa kuwa ni chaguo la wafanyabiashara kwa sababu anataka kupunguza na kuongeza uwekezaji na kuongeza thamani ya fedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.