rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani FBI Hillary Clinton

Imechapishwa • Imehaririwa

Ripoti: James Comey hakufuata utaratibu wa FBI

media
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa FBI James Comey Brendan Smialowski / AFP

Ripoti kutoka Wizara ya Sheria nchini Marekani, imeeleza kuwa aliyekuwa Mkuu wa Shirika la FBI James Comey hakufuata utaratibu mwaka 2016 alipokuwa anamchunguza mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton kuhusu madi ya kutumia anwani binafsi kufanya kazi za Wizara ya mambo ya nje.


Hata hivyo, ripoti hiyo imeonesha kuwa Bwana Comey hakuegemea upande wowote wa kisiasa wakati huo wa Uchaguzi.

Aidha, imebainika pia kuwa Bwana Comey alitumia anwani yake binafsi kufanya kazi za FBI, kinyume na utaratibu.

Pamoja na hilo, hatua ya Mkuu huyo wa zamani wa FBI kuanzisha uchunguzi dhidi ya Clinton wiki moja kuelekea Uchaguzi Mkuu imekosolewa katika ripoti hiyo.

Akijitetea, Comey alidokeza kuwa, alifanya hivyo kwa sababu ya kuonesha uwazi katika kazi yake.

Bi.Clinton ameendelea kumshtumu Bwana Comey kwa kumsababisha kushindwa na Donald Trump wakati wa Uchaguzi wa urais.