rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Canada Justin Trudeau

Imechapishwa • Imehaririwa

Marekani na Canada zalaumiana baada ya mkutano wa G7

media
Angela Merkel akizungumza na Donald Trump wakati wa mkutano wa nchi tajiri duniani, G7, huko La Malbaie, Juni 9, 2018. Bundesregierung/Jesco Denzel/REUTERS

Nchi ya Marekani inailaumu Canada kutokana na kumalizika vibaya kwa mkutano wa viongozi wa mataifa saba yenye nguvu ya kiuchumi duniani G7, nchi hiyo ikisema waziri mkuu Justin Trudeau amewasaliti Wamarekani huku Canada yenyewe ikiinyoshea kidole Washington.


Saa chache baada ya kutolewa kwa taarifa ya pamoja ya viongozi hao mwishoni mwa juma, rais Donald Trump kupitia mtandao wake wa Twitter alimshambilia waziri mkuu Trudeau na wakuu wengine wa nchi kwa kuinyonya nchi yake.

Hata hivyo waziri mkuu Trudeau amemjibu rais Trump akisisitiza nchi nyingine washirika ziko tayari kuchukua hatua dhidi ya tozo ya kodi ya bidhaa za Chuma na Aluminium iliyotangazwa na Marekani.

Wakuu wa nchi za G7 ni wazi safari hii walionekana kutofautiana vikali na Marekani huku rais Trump akiwahi kuondoka kabla ya kutamatika kwa mkutano wenyewe.