rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Korea Kaskazini Donald Trump Kim Jong Un

Imechapishwa • Imehaririwa

Trump aahidi kumwalika kiongozi wa Korea Kaskazini Washington

media
Rais wa Marekani, Donald Trump, Juni 7, 2018 katika ikulu ya White Maion. REUTERS/Carlos Barria

Ikiwa zimesalia siku chache kabla ya mkutano wa kihistoria wa Singapore kati ya Kim Jong-un na Donald Trump, rais wa Marekani amethibitisha nia yake ya kufikia suala la amani kutoka Korea Kaskazini.


Rais wa Marekani amebaini kwamba lengo hilo linaweza kufikiwa, ingawa amekiri kwamba pengine itachukua mikutano kadhaa kabla ya kutia saini kwenye mkataba. Kwa mara ya kwanza,amesemayuko tayari kumwalika kiongozi wa Korea Kaskazini mjini Washington.

Rais wa Marekani Donald Trump, amesema yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wiki ijayo nchini Singapore.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani pia amesema ana matumaini ya matokeo mazuri katika mkutano kati ya viongozi hawa wawili: "Kim Jong-un mwenyewe alinambia kuwa yuko tayari kuangamiza silaha zake za nyukila," amesema Mike Pompeo, bila kutoa maelezo zaidi.

"Marekani inataka maendeleo mazuri, sio maneno yasiyo na maana," ameonya Bw Pompeo. Aidha, Donald Trump amesema kuwa yuko tayari kuondoka meza ya mazungumzo ikiwa kutakua na hali ya sintofahamu katika mkutano huo. "Nilifanya hivyo mara moja, unapaswa kujua jinsi ya kususia jambo," alisema Donald Trump.

Kwa upande wake Japan inataka suala la wafungwa wa Kijapani liwekwe kwenye ajenda ya mazungumzo.

Trump amekutana na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, na kumwahidi kuwa atazungumzia pia kuachiliwa huru kwa raia wa Japan ambao wamezuiwa nchini Korea Kaskazini.