rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Guatemala Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Idadi ya vifo kufuatia mlipuko wa volkano yafikia 99 Guatemala

media
Ndugu wa Eric Rivas, kijana mwenye umri wa miaka 20 ambaye alipoteza maisha wakati wa mlipuko wa volkano ya Fuego, Guatemala. REUTERS/Jose Cabezas

Idadi ya vifo kufuatia mlipuko wa volkano inaendelea kuongezeka kila kukicha nchini Guatemala. Kwa mujibu wa serikali ya Guatemala idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia mlipuko huo imefikia 99.


Mlipuko huo umesababisha madhara makubwa kwa mara ya kwanza tangu miaka 40 iliyopita.

Watu karibu 200 hawajulikani waliko tangu mlipuko huo kuanza.

Mlipuko mpya wa volkano ya Fuego ulitokea Jumanne wiki hii, na kuwalazimu maafisa wa idara ya huduma za dharura kutafuta hifadhi na mamlaka kuwataka wakaazi kuondoka katika maeneo yaliyo karibu na volkano hiyo.

Mlipuko wa Volkano ya Fuego (Volkano ya moto), inayopatikana kilomita 35 kusini-magharibi mwa mji mkuu wa Guatemala, umesababisha maelfu ya watu kuhamishwa na uwanja wa ndege wa kimataifa umetakiwa kufungwa.