rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Colombia

Imechapishwa • Imehaririwa

Duru ya pili ya uchaguzi kufanyika Juni 17 Colombia

media
Mgombea urais Ivan Duque akiongea baada ya kutangazwa matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais Colombia, Mei 27, 2018. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins

Raia wa Colombia wanatarajiwa kushiriki katika Uchaguzi wa duru ya pili kumchagua rais mpya, baada ya matokeo kuonesha kuwa hakuna aliyepata asilimia 50 kama inavyohitajika kikatiba.


Kura zote zinaelekea kutamatishwa kuhesabiwa na mgombea wa mrengo wa conservative Ivan Duque anaongoza kwa asilimi 39.7 huku mpinzani wake Gustavo Petro akiwa na asilimia 24.8.

Ivan Duque aambaye anaongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Colombia uliyofanyika Jumapili wiki hii, baada ya kupata asilimia 39.1 ya kura atachuana katika duru ya pili na Gustavo Petro. Ivan Duque hakupata 50% ya kura iliyokua inahitajika ili kushinda uchaguzi huo. Duru ya pili imepangwa kufanyika Juni 17 mwaka huu. Gustavo Petro, kiongozi wa zamani wa waasi, alipata 25.1% na kuchukua nafasi ya pili. Naye Sergio Fajardo alipata 23.7% ya kura.

Mgombea wa mrengo wa kushoto katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Colombia: Jumapili, Mei 27, Gustavo Petro alipata 25% ya kura. REUTERS/Henry Romero

Katika nchi hii iliyokumbwa kwa zaidi ya nusu karne na vita vya wenyewe kwa wenyewe na ambako mrengo wa kulia unaendelea kushukilia utawala, kinara wa mrengo huo Ivan Duque, aliyepinga mkataba na waasi wa zamani, alimuangusha Gustavo Petro, Meya wa zamani wa Bogota, ambaye ni kutoa mrengo wa kushto, aliyejitenga na vyama vya kijadi. Wawili hawa watamenyana katika duru ya pili ya uchaguzi iliyopangwa kufanyika tarehe 17 Juni.

Iwapo mgombea wa mrengo wa Conservative atashinda, huenda mkataba uliosaidia kuletea amani kati ya serikai na waasi wa zamani wa FARC ukafanyiwa marekibisho suala ambalo limeanza kuzua wasiwasi nchini humo.