rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Chile Dini

Imechapishwa • Imehaririwa

Kashfa mpya ya unyanyasaji wa kijinsia yaikumba Kanisa Katoliki Chile

media
Kashfa hii mpya inaipaka matope kanisa la Katoliki nchini Chile baada ya kujiuzulu kwa Maaskofu wote katika nchi hiyo kwa kashfa za unyanyasaji wa kijinsia. REUTERS/Ivan Alvarado

Baada ya kujiuzulu kwa Maaskofu wote nchini Chile siku ya Ijumaa kwa kashfa ya unyanyasaji wa kingono katika miaka ya hivi karibuni, Mapadri wanashtumiwa kuwanyanyasa kingono watoto. Hii ni kashfa mpya inayoendelea kulikumba kanisa Katoliki katika nchi hiyo.


Mapadri kumi na wanne wa dayosisi ya Rancagua wamesimamishwa kazi na Kanisa katika siku za hivi karibuni.

Jumla ya Mapadri 14 wa dayosisi wamesimamishwa kazi, fursa kwa Kanisa la Chile kuchunguza ukweli kuhusu matukio yaliyoshtumiwa na kituo cha televisheni cha serikali.

Wengi wao, ikiwa ni pamoja na mkuu wa shule ya msingi ya Katoliki, wanashtumiwa unyanyasaji wa kingono kwa watoto, au pia kutuma picha za ngono kwa vijana.Maaskofu 34 wa Chile, ambao waliitishwa wiki jana Vatican kwa mkutano wa kujadili mgogoro kuhusu kashfa za unyanyasaji wa kingono, waliwasilisha barua yao ya pamoja ya kujiuzulu kwa Papa Francis, kulingana na taarifa iliyotolewa Ijumaa wiki hii.

Wakati wa ziara yake nchini Chile mnamo mwezi Januari mwaka huu, Papa Francis alimtetea Askofu Juan Barros, akwa kuficha visa vya unyanyasaji wa kijinsia katika Kanisa la Chile.

Kwa matokeo ya uchunguzi huu, Papa mwezi uliopita alikiri kuwa amefanya "makosa makubwa" kwa jinsi alivyoshughulikia kesi hii kwa sababu alikosa "taarifa za kuaminika na zenye usawa".