Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MADURO-UCHAGUZI-SIASA

Nicolas Maduro ashinda uchaguzi wa urais Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika hapo jana, uchaguzi ambao mgombea wa upinzani aliyeshiriki amesema ulikuwa batili na kutaka kuitishwa kwa uchaguzi mkuu mpya.

Rais wa Venezuela akisabahi wafuasi wake baada ya 'kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Mei 20, 2018, Caracas.
Rais wa Venezuela akisabahi wafuasi wake baada ya 'kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Mei 20, 2018, Caracas. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Ni asilimia 46 pekee ya wapiga kura walijitokeza katika uchaguzi ambao ulisusiwa na muungano wa upinzani na kukashifiwa vikali na jumuiya ya kimataifa lakini ndio uchaguzi unaompa muhula mwingine wa miaka 6 rais Maduro.

Venezuela inaendelea kukabiliwa na hali tete ya uchumi.

Mgombea pekee wa upinzani Henri Falcon amewaambia wanahabari mjini Caracas kuwa hatambui matokeo ya uchaguzi huo aliosema haukuwa huru wala haki.

Hata hivyo rais Maduri akihutubia maelfu ya wafuasi wake muda mfupi uliopita, amepongeza ushindi wake ambao amesema ni wakihistoria kwa mgombea kupata asilimia 68 ya kura zote.

Matokeo yanampa rais Maduro ushindi wa asilimia 67.7 huku mpinzani wake falcon akipata asilimia 21.2.

Wagombe wawili wa upinzani walizuiliwa kushiriki huku baadhi wakiendelea kuzuiliwa kwenye jela za nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.