rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nicaragua

Imechapishwa • Imehaririwa

Maaskofu kutafutia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa Nicaragua

media
Raia wakiandamana dhidi ya serikali NIcaragua. REUTERS/Oswaldo Rivas

Baraza la Maaskofu nchini Nicaragua limetangaza kuwa linajiandaa kuwa msuluhishi wakati wa mazungumzo kati ya serikali na wawakilishi wa mashirika ya kiraia.


Mazungumzo hayo yanatarajia kuanza Jumatano wiki hii baada ya maandamano yaliyosababisha vifo vingi katika wiki za hivi karibuni dhidi ya Rais Daniel Ortega.

Mazungumzo haya yaliitishwa saa chache baada ya Tume ya Haki za Binadamu kutoka Jumuiya ya nchi za Amerika ya Kati (IACHR), shirika linalojikita katika masuala ya unyanyasaji, mateso na visa vya watu kutoweka katika bara la Amerika, kutangaza kwamba lilialikwa nchini Nicaragua kwa uchunguzi.

Maandamano dhidi ya serikali yalianza katikati ya mwezi Aprili kufuatia mageuzi tata katika nyanja ya kijamii. Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa uliripoti vifo vya watu wasiopungua 47, wengi wao wanafunzi.

Waandamanaji pia wameomba kujiuzulu kwa Rais Ortega, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi anayeshtumiwa kutaka kuanzisha utawala wa kifamilia katika nchi hiyo ya Amerika ya Kati.

Baraza la Maaskodu nchini Nicaragua linasema katika taarifa kwamba litachukua nafasi ya mpatanishi na shahidi katika mazungumzo, kwa lengo la kuzileta pande zinazokinzana kwenye makubaliano.

Awali, Luis Almagro, Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Amerika ya Kati, inayojumuisha IACHR, aliweka kwenye ukurasa wake wa Twitter barua ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Nicaragua Denis Moncada, ikialika IACHR nchini.

Barua hiyo haijaeleza tarehe ambayo ziara hiyo itafanyika.