rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Maelfu ya wakazi wa Hawaii wayahama makazi yao kufuatia mlipuko wa volkano

media
Moshi mkubwa ukisababishwa na volkano Kilauea huko Hawaii tarehe 3 Mei 2018, kwenye picha iliyopigwa na Janice Wei AFP

Mlipuko wa Volkano Kilauea, moja ya volcano zinazoendelea kuhatarisha maisha ya binadamu duniani, umeathiri maeneo ya makazi ya jimbo Hawaii, nchini Marekani. Mlipuko huu umesababisha maelfu ya wakazi wa jimbo hilo kukimbia makwao kuepuka madhara.


Gavana David Ige ametangaza hali ya dharura ili kuhamasisha idara mbalimbali za serikali na kukusanya fedha za dharura zinazohusiana na majanga ya asili.

Afisa mmoja wa eneo hilo amesema kuwa karibu watu 10,000 wanaoishi eneo hilo wameanza kuhamishwa kwenda maendo salama.

Majengo 770 na watu 1,700 wametakiwa kuhama haraka, Cindy McMillan, msemaji wa Gavana David Ige ameliambia shirika la habari la AFP.

Vituo viwili vya mapokezi vimefunguliwa ili kuwapokea watu wanaohamishwa. Gavana wametolea wito kikosi cha ziada kuja kusaidia shughuli za uokoaji, McMillan amebaini kwenye ukurasa wake wa Twitter. "Jitayarisheni sasa ili familia zenu ziwe salama," gavana amewaambia wakazi wanaokabiliwa na opresheni hiyo ya kuhamishwa kwa nguvu.