rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Korea Kaskazini Donald Trump Kim Jong Un

Imechapishwa • Imehaririwa

Trump: Tunajiandaa kwa mazungumzo na Korea Kaskazini

media
Ni nyumbani kwake huko Mar-a-Lago, Florida, ambapo Donald Trump alimpokea Shinzo Abe, Waziri Mkuu wa Japan. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kuwa kutakuwa na mazungumzo ya moja kwa moja kati ya serikali yake na ile ya Korea Kaskazini.


Trump amesema hayo wakati akikutana na Waziri Mkuu wa Japam Shinzo Abe anayezuru Marekani kwa ziara ya kikazi.

Kiongozi huyo wa Marekani ameongeza kuwa anatoa baraka zake, ili kufanikiwa kwa mazungumzo hayo ili kumaliza mvutano wa miaka mingi na vita vya kidiplomasia kati ya Korea Kaskazini na Mataifa jirani bila kusahu Marekani.

Aidha, ameongeza kuwa kufanikiwa kwa mazungmzo hayo kutasaidia kumalizika kwa vita kati ya Korea Kaskazini na Kusini, vita ambavyo amesema bado vinaendelea.

Ripoti ya Gazeti la The Washington Post imeeleza kwamba aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la CIA Mike Pompeo tayari alikutana kwa siri na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alipofanya ziara ya siri jijini Pyongyang mwezi Aprili, alipoteuliwa tu kuwa Waziri wa Mambo ya ndani.

Wakati hayo yakijiri, ripoti kutoka Seoul zinasema kuwa, Korea Kusini inataka kupata mwafaka wa kudumu na jirani yake Korea Kaskazini ili kumaliza mvutano wa muda mrefu na vitisho vya usalama hasa kutokana na mradi wa nyukilia wa Pyongyang.