rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Brazili Luiz Inacio Lula da Silva

Imechapishwa • Imehaririwa

Mahakama Kuu kumuachilia huru rais wa zamani wa Brazil

media
Majaji wa Mahakama Kuu ya Brazil wakijadili uamuzi wa kuchukua kuhusu kesi ya rais wa zamani wa Brazil Lula da Silva, tarehe 4 Aprili, 2018 Brasilia. AFP

Jaji wa Mahakama Kuu ya Brazil ameomba kuahirishwa hadi wiki ijayo kwa mjadala uliopangwa kufanyika Jumatano wiki hii ambao ungeweza kuplekea kuachiliwa huru kwa rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva, anayezuiliwa jela tangu jumatano iliyopita.


Mvutano umeendelea nchini Brazil kufuatia kesi hiyo na tayari kumeanza kujitokeza mgawanyiko katika serikali ya nchi hiyo kufuatia uamuzi wa mahaka kumuweka jela rais huyo wa zamani

Jaji Marco Aurelio de Mello alikubali ombi la chama kidogo cha mrengo wa kulia cha PEN, kwa hatua ya utaratibu, ambayo iliomba uamuzi wa mahakama kuahirishwa kwa siku tano .

Uamuzi huu ni njia ya kufungua mjadala juu ya kanuni ya utekelezaji wa hukumu tangu kukataliwa kwa rufaa ya kwanza, hata kama rufaa nyingine bado zinawezekana.

Jaji anayehusika na kesi za rushwa nchini Brazil, Sergio Moro alimhukumu Lula mara ya kwanza mnamo mwezi Julai, hukumu iliyothibitishwa na Mahakama ya Rufaa katikati ya mwezi wa Januari. Usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki iliyopita, Mahakama Kuu ya Brazil ilikataa ombi la Lula da Silva ambalo lingeweza kumruhusu rais huyo wa zamani (2003-2010) kubaki huru mpaka kukamilika kwa taratibu zote za kisheria.

Lula, mwenye umri wa miaka 72, alihukumiwa kwa kosa la kupokea ghorofa ya kifahari ilio pembezoni mwa bahari kutoka kampuni ya ujenzi baada ya kupewa zabuni.

Kiongozi huyo wa mrengo wa kushoto, ambaye pia anakabiliwa na kesi sita, amekanusha tuhuma hizo dhidi yake, akielezea ukosefu wa ushahidi na mpango wa kumzuia kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba, uchaguzi ambao anapewa nafasi kubwa ya kushinda.