Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-DIPLOMASIA

Wanadiplomasia 60 wa Marekani waondoka Urusi

Wanadiplomasia 60 wa Marekani ambao wamefukuzwa kutoka Nchini Urusi baada ya sakata la sumu inayodaiwa ilipewa jasusi wa zamani Serguei Skripal na binti yake wameondoka katika ubalozi wa Washington huko Moscow mapema leo Alhamisi asubuhi.

Ubalozi wa Marekani Moscow, Urusi.
Ubalozi wa Marekani Moscow, Urusi. REUTERS/Tatyana Makeyeva
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wa shirika la habari la AFP Alieyeko Moscow ameshuhudia kuuona msafara wa mabasi matatu ya ubalozi wa Marekani pamoja na magari mengine yakielekea kwenye uwanja wa kimataifa alfajiri hii.

Hatua hii inakuja baada ya Moscow kuweka tarehe ya leo Alhamisi Aprili 5 kuwa tarehe ya mwisho kwa wanadiplomasia wa Marekani wawe wameondoka nchini humo.

Wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, alisema nchi yake itawafukuza nchini humo wanadiplomasia 60 wa Marekani na kufunga ofisi za ubalozi wake mjini Saint Petersburg kujibu kitendo cha wanadiplomasia wake kufukuzwa na nchi za Magharibi.

Utawala wa Washington wenyewe umesema kuwa kitendo kilichofanywa na Urusi hakina msingi wowote na kwamba Serikali inafikiria hatua nyingine za kuchukua.

“Ni wazi kutokana na orodha tuliyokabidhiwa kuwa Urusi haiko tayari kwa mazungumzo ya masuala yanayozikabili nchi hizi mbili,” amesema msemaji wa wizara ya mambo ya nje Heather Nauert.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.