Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISRAEL-UBALOZI-JERUSALEM

Trump huenda akashuhudia kufunguliwa kwa Ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem

Rais wa Marekani Donald Trump amesema huenda akasafiri kwenda nchini Israel mwezi Mei kushuhudia Ubalozi wa nchi hiyo ukihamishwa kutoka mjini Tel Aviv kwenda mjini Jerusalem.

Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuui Benjamin Netanyahu, wakiwa mbele ya Ikulu ya Marekani
Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuui Benjamin Netanyahu, wakiwa mbele ya Ikulu ya Marekani REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Trump ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya White House jijini Washington DC.

Netanyahu amesema hatua ya Marekani, haitasahaulika kamwe katika historia ya nchi yake.

Uamuzi wa Marekani umeikera Palestina ambayo imesema hatua hiyo haikubaliki kamwe.

Hatua ya Marekani imezua wasiwasi wa iwapo, kutakuwa na matumaini tena ya kuanzisha mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel.

Jerusalem ni mji Mtakatifu kwa nchi hizo mbili kiimani na kihistoria huku kila mmoja akisema Mashariki mwa mji huo ni eneo lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.