Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Trump apendekeza walimu kupewa silaha kuzuia mauaji shuleni

Rais wa Marekani Donald Trump anataka hatua kali zichukuliwe ili kuzuia mauaji katika shule na kupendekeza kama njia inayowezekana kwa walimu na wafanyakazi wengine wa shule kupewa silaha ili kukomesha mauaji hayo.

Maandamano katika mitaa mbalimbali ya Florida baada ya shambulio lililogharimu maisha ya wanafunzi 17 katika shule ya sekondari ya Parkland, mauaji ambayo yaliibua mjadala mkubwa ya udhibiti wa mauzo ya silaha nchini Marekani.
Maandamano katika mitaa mbalimbali ya Florida baada ya shambulio lililogharimu maisha ya wanafunzi 17 katika shule ya sekondari ya Parkland, mauaji ambayo yaliibua mjadala mkubwa ya udhibiti wa mauzo ya silaha nchini Marekani. REUTERS/Mike Blake
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amerejelea pendekezo hili la National Rifle Association (NRA), taasisi ku inayohusikamna kuchunguza udhibiti wa silaha nchini Marekani, wakati mamia ya watu, ikiwa ni pamoja na waathirika wa mauaji ya hivi karibuni ya Parkland, Florida, kuandamana katika mitaa mbalimbali wiki moja baada ya mauaji ya wanafunzi 17 wa shule ya sekondari ya Parkland.

Katika miji ya Washington, Chicago na Pittsburg, hasa, maandamano mengine yalifanyika siku ya Jumatano.

Mauaji haya ambayo ni kisa cha 18 cha aina yake tangu mwanzoni mwa mwaka huu nchini Marekani, lakini mauaji mabaya baada ya yale yaliyotokea katika shule ya msingi ya Sandy Hook, huko Newtown, Connecticut, mnamo mwezi Desemba 2012, yaliibua mjadala mkubwa juu kudhibiti uuzaji wa silaha.

Mwuaji wa Parkland ni Nikolas Cruz, kijana mwenye umri wa miaka 19, ambaye aliweza kupewa silaha alipokamilisha umri wa kumiliki silaha mwaka jana.

Maelfu ya watu walijitokeza ili kumuomba Rais Donald Trump kutoa msimamo wake juu ya suala hili. Rais wa Marekani, mtetezi shupavu wa Marekebisho ya Pili ya Katiba ambayo inalinda haki ya milki ya silaha, aliandaa "mkutano" na wazazi, wanafunzi na walimu jana Jumatano katika ikulu ya White House.

Aliahidi kuimarisha sheria zinazohusu ukaguzi wa watu wanaomiliki silaha kwa mujibu wa sheria.

Hatutokubali watu kupewa silaha kiholela, hatutokubali kamwe, Rais Trump alisema.

"Hatuwezi kusem abila kutenda kama zamani," aliongeza.

Hata hivyo Donald Trump pia alipendekeza walimu na wafanyakazi wengine waweze kupewa silaha, kwa masharti kwanza wapewe mafunzo sahihi ya kutosha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.