rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Korea Kaskazini Mike Pence

Imechapishwa • Imehaririwa

Marekani kukutana kwa mazungumzo na Korea Kaskazini bila masharti

media
MAkamu wa rais wa Marekani Mike Pence. REUTERS/Ammar Awad

Marekani kupitia Makamu wa rais wa nchi hiyo Mike Pence imesema kuwa iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote.


Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, likimnukuu Bw Pence, ikiwa Korea Kaskazini inataka mazungumzo, basi utawala wa Trump utafanya hivyo, na hakutakuepo na masharti.

Awali utawala wa Trump ulisema kuwa hautafanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon-un ikiwa tu yuko tayari kuachana na mpango wa nyuklia.

.Wadadisi wanasema Marekani imebadilisha msimamo wake dhidi ya Korea Kaskazini baada ya kuonekana kuwa haina ushawishi mkubwa wa kuizuia nchi hiyo kuendelea mpango wake wa silaha za nyuklia.

Hivi karibuni Marekani ilitishia kuivamia kijeshi Korea Kaskazini, ikiionya kuwa itasambaratishwa kama haitaki kuachana na mpango wake wa silaha za nyukilia na kufanya majaribio yake ya makombora ya masafa marefu.

Hata hivyo Makamu wa rais wa Marekani amesema akisisitiza kuwa vikwazo vitakuwepo hadi pale Korea Kaskazini itachukua hatua za kumaliza mpango wake wa silaha za nyuklia.