Pata taarifa kuu
VENEZUELA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi mkuu kufanyika Aprili 22 Venezuela

Baraza la uchaguzi nchini Venezuela limetangaza kuwa uchaguzi mkuu wa urais nchini humo utafanyika tarehe 22 ya mwezi April, uchaguzi ambao upinzani unamtuhumu rais Nicolas Maduro kwa kujiandalia kutawala kwa muhula wa pili.

Rais anayemaliza muda wake nchini Venezuela, Nicolas Maduro, ni mgombea katika uchaguzi wa Aprili 22, 2018.
Rais anayemaliza muda wake nchini Venezuela, Nicolas Maduro, ni mgombea katika uchaguzi wa Aprili 22, 2018. REUTERS/Marco Bello
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo, Tibisay Lucena, ametoa tangazo hilo hapo jana Jumatano baada ya kuvunjika kwa mazungumzo kati ya Serikali na upinzani katika kukubaliana tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Wakati huu ambapo muungano wa upinzani umekataliwa kusimamisha mgombea na baadhi ya wakosoaji wakubwa wa rais Maduri kuzuiwa, tayari watu wameonesha hofu ya rais Maduro kutumia mwanya huo kujiandalia mazingira ya kuendelea kutawala.

Nchi ya Venezuela ilikuwa iandae uchaguzi mkuu wa rais ifikapo mwezi Desemba mwaka huu lakini jitihada za rais Maduro kutumia bunge alilounda amefanikiwa kurudisha nyuma tarehe ya uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.