rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Wahamiaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Trump kuwapa uraia zaidi ya watu Milioni mbili Marekani

media
Maandamano karibu na ikulu ya White House Septemba 5, 2017 dhidi ya uamuzi wa Donald Trump wa kusitisha ulinzi wa wahamiaji haramu waliowasili wakiwa vijana nchini Marekani, wanaojulikana kama "Dreamers". REUTERS/Aaron P. Bernstein

Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa, rais Donald Trump anapanga kuwapa uraia zaidi ya watu Milioni mbili ambao wamekuwa wakiishi nchini humo bila vibali halali.


Hili limekuja baada ya chama cha Republican kupanga kuwasilisha mswada wa kuomba Dola Bilioni 25 ili kujenga ukuta katika mpaka na Mexico.

Wasaidizi wa karibu wa Trump wanasema, wahamiaji hao watapewa uraia na kuwasihi wabunge wa upinzani wa Democratic kuunga mkono mpango a kujenga ukuta huo, lakini wapinzani wamesema hawawezi kukubali.

Mvutano kuhusu matumizi ya shughuli za serikali uliokua uliibuka nchini marekani, ulimalizika baada ya bunge la Seneti kupitisha matumizi ya muda kufadhili shughuli hizo.

Baada ya mazungumzo mengi, viongozi wa chama cha Democratic katika baraza la Seneti walikubali muswada huo ambao utasaidia kufadhili huduma za serikali hadi februari 8, kwa lengo lililowekwa la kufikia mkataba kuhusu hatima ya mamia ya maelfu ya wahamiaji haramu waliowasili wakiwa vijana nchini Marekani, wanaojulikana kama "Dreamers".

Wawakilishi wa chama cha Democratic walisema kuwa wataunga mkono muswada huo kama utatoa hatma ya maelfu ya wahamiaji waliongia Marekani wakiwa watoto ambapo sasa wanakabiliwa na hatua ya kurudishwa sehemu walizotoka.