rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani

Imechapishwa • Imehaririwa

Daktari wa timu ya Olimpiki Marekani ahukumiwa jela miaka 175

media
Wasichana na wanawake 160, walijitokeza kutoa ushahidi dhidi ya daktariLarry Nasser, ambaye juhudi zake za kuomba radhi hazikuzaa matunda. REUTERS/Fabrizio Bensch

Aliyekuwa Daktari wa timu ya taifa ya akina dada ya michezo ya kuruka hewani nchini Marekani Larry Nasser, amehukumiwa kifungo cha miaka 175 jela.


Nasser mwenye umri wa miaka 54, amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na makosa 10 ya kuwanyanyasa kimapenzi mamia ya wanamichezo wa kike, ambao walijitokeza kutoa ushahidi.

Wasichana na wanawake 160, walijitokeza kutoa ushahidi dhidi ya daktari huyo ambaye juhudi zake za kuomba radhi hazikuzaa matunda.

Jaji Rosemarie Aquilina amesema daktari huyo ni mtu hatari.

“Najisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na nataka iwe fundisho kwa wengine, “ Jaji Rosemary Aquilina ameiambia mahakama.

Takriban wasichana 140 wamewasilisha kesi dhidi ya Nasser, taasisi ya USA Gymnastics na chuo kikuu cha MSU, wakidai kuwa taasisi hizo mbili zilipokea tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya daktari huyo miaka kadhaa ya nyuma.

Wakati huo huo mkuu wa chuo kikuu cha jimbo la Michigan (MSU) alikokuwa anafanya kazi Nasser kati ya mwaka 1997 na 2016, amejiuzulu.

Lou Anna Simon amekuwa akikabiliwa na shinikizo kujiuzulu.