rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Donald Trump Afya

Imechapishwa • Imehaririwa

Daktari wa Trump asema rais Trump hana matatizo ya kiakili

media
Wiki iliyopita Trump alifanyiwa uchunguzi wa afya wa saa tatu, ambao ni uchunguzi wa kwanza tangu achukue hatamu ya uongozi wa nchi ya Marekani. REUTERS/Jim Bourg

Daktari wa rais wa Marekani Donald Trump amesema, kiongozi huyo ana afya njema na inatarajiwa kuwa ataendelea hivyo kipindi chake chote cha urais.


Daktari huyo Ronny Jackson ametoa taarifa hii baada ya kumfanyia uchunguzi wa kiafya rais Trump ambaye alingia madarakani mwaka uliopita.

“Rais Trump hajaonyesha dalili zozote za matatizo ya kiakili kufuatia uchunguzi wa kiafya na yuko la afya nzuri, “ daktari Ronny Jackson amesema.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano huko White House, Daktari Jackson amesema kuwa kwa jumla afya ya rais ni nzuiri.

Kumekuwa na wasiwasi kuwa, huenda rais Trump anasumbuliwa na matatizo ya akili kutokana na matamshi na maamuzi ambayo amekuwa akiyatoa tangu alipoingia madarakani.