rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Donald Trump Wahamiaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Trump ashambulia kwa matusi mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador

media
Donald Trump katika katika ikulu ya White House tarehe 10 Januari 2018. REUTERS/Carlos Barria

Ubaguzi wa rangi umeendelea kuonekana katika matamshi ya rais wa Marekani Donald Trump ambaye alizitaja nchi za Haiti, El Salvador, pamoja na mataifa kadhaa ya Kiafrika kuwa ni "nchi chafu".


Rais alitoa kauli hiyo wakati ambapo maseneta walikua wakimuonyesha makubaliano walioyafikia kuhusu wahamiaji. Maseneta wengi kutoka vyama vya Republican na Democrats walionyesha hasira yao.

Vyanzo kadhaa viliripoti tukio hilo na ikulu ya White House haikukanusha. Maseneta walikuwa katika ofisi ya rais wakiwasilisha makubaliano waliofikia kuhusu wahamiaji.

Maseneta wa chama cha Republican waliweka ukomo kwa kuunganisha familia, kama mwisho wa bahati nasibu ili kupata kadi ya kijani, na hatua za usalama kwenye mipaka. Maseneta wa chama cha Democrat walipata upanuzi wa haki ya kuishi nchini Marekani kwa vijana waliowasili nchini humo wakiwa watoto na kuongezwa kwa muda wa sheria ya ulinzi kwa raia wa Haiti na El Salvador.

Wakati huo rais Donald Trump alisema, akimaanisha raia wa Kiafrika: "Kwa nini watu wote kutoka nchi chafu wanaendelea kuja hapa? ".

Roberto Lopez, Naibu kiongozi wa chama cha wafanyabiashara kutoka El Salvador nchini Marekani, amesema ameshangazwa na kauli hiyo. "Ni hatari, ni hatari ... Ninamaanisha, hiyo siyo lugha ya kutumia. Nilitarajia kitu kingine kutoka kwa rais wa Marekani, kutoka kwa kiongozi wa ulimwengu wa utandawazi. Ni ajabu kuona alitoa kauli hiyo ", alise aalipokua akihojiwa na RFI.

Maseneta wengi walitoa misimamo yao baada ya kauli hiyo ya Donald Trump. Mia Love, mwakilishi wa chama cha Republican mwenye asili ya Haiti amesema: "Hii inakiuka maadili ya kitaifa. Mwenendo huo haukubaliki kwa mtu kama kiongozi wa nchi yetu. "