rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Bannon ajiuzulu kutoka Shirika la Habari la Breitbar

media
Steve Bannon, wakati wa kampeni katika nyumba ya trump ya Trump Tower, New York, Agosti 20, 2016. REUTERS/Carlo Allegri

Aliyekuwa mkuu wa masuala ya mikakati katika Ikulu ya Marekani Steve Bannon amejiuzulu kutoka shirika la habari la Breitbart kutokana na kashfa kutoka kwa rais Donald Trump.


Hatua hii inakuja baada ya kunukuliwa katika kitabu kinamchomzugumzia rais Trump.

Katika kitabu hicho kilichopewa jina"Fire and Fury, Bannon ananukuliwa akisema Trump anaonekana kuwa na matatizo ya akili na asiyefuatilia mambo kwa kina, madai ambayo Trump ameyakanusha.

Rais wa Marekani Donald Trump alijaribu kuzuia kuchapishwa kwa kitabu hiki chenye utata ambacho hatimae kiliwekwa sokoni lsiku ya Ijumaa Januari 5 mwaka huu.

Siku ya Alhamisi wanasheria wa Donald Trump waliomba kitabu hicho kisichapishwi, na kutishia kumfungulia mashitaka mchapishaji wa kitabu hicho. Wanasheria wa Trump wanachukulia kuhusu maelezo ya kitabu hicho, ambapo Michael Wolff anakubali kwamba "mengi ya habari kuhusu kile kilichotokea katika ikulu ya White House zinatafautiana.

Hayao yanajiri wakati ambapo Robert Mueller anayeongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani anatarajiwa kumhoji rais Trump hivi karibuni.

Mawakili wa rais wa Marekani Donald Trump wanashauriana na wachunguzi wanaotarajia kumhoji Trump, kuhusu anachokifahamu kuhusu madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani mwaka 2016.

Rais Trump na wale wote waliomsaidia kipindi cha kampeni wameendelea kukanusha madai kuwa walishirikiana na Urusi, kumsaidia kushinda urais.

Urusi pia imekanusha madai hayo. Lakini washirika wa karibu wa zamani wa Donald Trump wameendelea kuhakikisha kuwa kulikuepo na mikutano iliyofanyika mara kadhaa kati ya maafisa wa Urusi na ndugu na washirika wa karibu wa Bw Trump.

Haitakuwa mara ya kwanza rais wa Marekani kuhojiwa na mahakama akiwa madarakani. Bill Clinton alitakiwa kujieleza kuhusu tuhuma za ngono katika kesi ya Lewinsky na George Bush alihojiwa katika ofisi ya mashitaka kuhusu kutoa utambulisho wa afisa wa shirika la ujasusi la CIA.