Pata taarifa kuu
PERU-AJALI-USALAMA

Watu 48 wafariki dunia katika ajali ya basi Peru

Watu wasiopungua 48 walipoteza maisha siku ya Jumanne katika ajali ya basi iliyoanguka baada ya kugongana na lori nchini Peru. Ajali hii ilitokea kwenye barabara kuu kando ya pwani ya Pasifiki, polisi imesema.

Picha ya shirika la habari la Peru la Andina ikionyesha waokoaji, polisi na maafisa wa Zima Moto wakilizungka basi lililofanya ajali karibu na Pasamayo, kaskazini mwa Lima, na kuua watu wasiopungua 48 Januari 2, 2018.
Picha ya shirika la habari la Peru la Andina ikionyesha waokoaji, polisi na maafisa wa Zima Moto wakilizungka basi lililofanya ajali karibu na Pasamayo, kaskazini mwa Lima, na kuua watu wasiopungua 48 Januari 2, 2018. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 48," polisi imesema katika taarifa iliyorushwa kwenye tovuti ya wizara ya mambo ya ndani ya Peru, ambayo ilisema zoezi la kutoa miili ndani ya basi ilisimama wakati wa usiku kwa sababu ya mawimbi yenye nguvu kutokana na hali mbaya ya hewa.

Ripoti ya awali ilibaini watu 36 walifariki dunia katika ajali hiyo.

Ajali hiyo ilitokea saa 11:43 saa za Peru kilomita 45 kaskazini mwa mji mkuu Lima, Mkuu wa polisi ya barabarani, Kanali Dino Escudero, amewaambia waandishi wa habari.

Kulikuwa na abiria 55 na madereva wawili ndani ya basi ambayo ilikuwa inaelekea mji mkuu wa Peru kutoka mji wa Huacho (katikati mwa nchi) kilomita 130.

Abiria sita pekee walipatikana wakiwa hai na wamelazwa hospitalini, huku wanne kati yao wakiwa katika hali mbaya.

Basi hilo lilianguka kwenye umbali wa zaidi ya mita mia moja karibu na bahari.

Wokoaji, ambao baadhi yao walisaidiwa na helikopta kufika eneo la ajali na wengine walishuka kwa kutumia kamba, walisitisha zoezi hilo wakati wa usiku kwa sababu ya mawimbi ya bahari. Zoezi hilo linatarajia kuendelea leo Jumatano, kwa mujibu wa Naibu Mkuu wa kikosi cha Zima Moto.

 

"Ni masikitiko kwa nchi kukumbwa ajali hii mbaya. Ninaungana na familia zilizopoteza ndugu zao," Rais Pedro Pablo Kuczynski ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.