Pata taarifa kuu
COSTA RICA-USALAMA-AJALI

Watu 12 wafariki katika ajali ya ndege Costa Rica

Watu 12 ikiwa ni pamoja na 10 raia wa Marekani wamefariki katika ajali ya ndege magharibi mwa Costa Rica, rubani na rubani msaidizi walikua ni raia wa Costa Rica.

Moja ya mitaa ya mji wa San Jose, Costa Rica, ambapo ndege iliyokua ikibeba watalii 10 raia wa Marekaniilio kua ikitokea ikielekea Punta Islita,, ilianguka.
Moja ya mitaa ya mji wa San Jose, Costa Rica, ambapo ndege iliyokua ikibeba watalii 10 raia wa Marekaniilio kua ikitokea ikielekea Punta Islita,, ilianguka. REUTERS/Juan Carlos Ulate
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Costa Rica amethibitisha ajali hiyo katika taarifa iliyochapishwa mitandaoni akisema kuwa serikali yake imesikitishwa sana na vifo hivyo.

Mtangulizi wake rais wa zamani Laura Chinchilla, aliandika katika mtandao wa Twitter kuwa mmoja wa wahudumu wa marubani alikuwa ni binamu wake.

Ripoti zinasema kuwa ndege hiyo ya injini moja ya Cessna 208 Caravan, ilikuwa safarini kutoka mji mkuu San José kwenda Punta Islita ambalo ni eneo la kistarehe.

Mpaka sasa haijabainika chanzo cha ajali hiyo. Watu wote waliokuemo katika ndege hiyo ndogo walifariki.

Vyombo vya habari vimesema kuwa watano kati ya wale waliofariki katika ajali hiyo ni kutoka familia moja.

Hivi karibuni Costa Rica ilikumbwa na kimbunga Nate, kilichosababisha vifo vya watu wengi huku watu 400,000 wakiachwa bila makazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.