Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-CHINA

Urusi, China zakosoa mkakati wa rais Trump kuhusu usalama wa taifa

Serikali za Urusi na China zimekosoa vikali hotuba ya rais wa Marekani Donald Trump aliyoitoa wakati akieleza mkakati wake kuhusu usalama wa taifa.

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. 路透社
Matangazo ya kibiashara

Kwenye hotuba yake rais Trump alizigusa nchi za China na Urusi kama mataifa ambayo yanaleta ushindani kwa nchi yake na ndio tishio kwa ustawi wa uchumi wake.

Msemaji wa rais Vladimir Putin, Dmitry Peskov amekosoa mkakati wa rais Trump kuhusu usalama wa taifa akisema nchi hiyo inatafuta umaarufu ambao hauna maana kwa dunia ya sasa.

Serikali ya China kwa upande wake imesema kilichoainishwa na Marekani ni vita baridi ya kiakili inayolenga kujaribu kuleta sintofahamu ya usalama wa dunia.

Rais Trump alikuwa akizindua mkakati wake wa kwanza wa usalama wa taifa wenye kurasa 68 unaoelezea mipango ya utawala wake tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani huku akiusifu uhusiano baina ya Marekani na Urusi.

Tangu alipoingia madarakani Januari 20 mwaka huu, Trump amekuwa akisisitiza sera ya Marekani kwanza ambayo ilikuwa agenda yake kuu wakati wa kampeni za uchaguzi.

Hivi karibuni Shirika la ujasusi la Marekani lilifanikiwa kutoa taarifa nyeti zilizozuia kutokea kwa shambulizi la kigaidi katika kanisa la Saint Petersburg lililo jirani na makazi ya rais wa Urusi, Vladmir Putin.

Chapisho lililoibuliwa hivi karibuni limemnukuu Trump akiyataja mataifa ya Urusi na China kuwa yanatoa chanamoto kwa maslahi na ushawishi wa Marekani kwa washirika wake zikilenga kuharibu usalama wa Marekani

Matamshi ya kiongozi huyo wa taifa hilo linaloongoza kwa nguvu za kiuchumi na kijeshi duniani, yanakuja wakati maofisa wa Marekani wakiendelea na uchunguzi juu ya madai kuwa Trump alisaidiwa na maofisa wa Urusi katika kampeni za uchaguzi za mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.