rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Nikki Haley Donald Trump UN Palestina Ufaransa Italia Uingereza

Imechapishwa • Imehaririwa

Marekani yatumia kura ya turufu kuzua azimio la UN kuhusu Jerusalem

media
L'ambitieuse ambassadrice des Etats-Unis aux Nations unies pendant l'Assemblée générale de l'organisation, le 21 septembre 2017, à New York. REUTERS/Stephanie Keith

Nchi ya Marekani imetumia kura yake ya turufu kuzuia azimio la baraza la usalama la umoja wa Mataifa lililotaka kupinga uamuzi wa nchi hiyo kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu wa Israel licha ya azimio hilo kuungwa mkono na nchi nyingine 14 wanachama.


Kura hiyo ilipigwa na balozi wa Marekani kwenye umoja huo Nikki Haley ambaye amesema kitendo kilichofanywa na nchi nyingine ni cha aibu na kwamba kuna siku watajutia uamuzi walioufanya kwa kuwa Marekani ilichofanya ni kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv.

Uamuzi wa rais Trump alioufanya mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu kulivunja makubaliano ya jumuiya ya kimataifa kuhusu suluhu kati ya Israel na Palestina hali iliyosababisha maandamano.

Nchi washirika na Marekani kama vile Ufaransa, Uingereza, Japan , Italia na Ukraine zilikuwa ni miongoni mwa mataifa mengine 14 wanachama wa baraza la usalama waliounga mkono azimio lililowasilishwa na Misri.

Azimio hili lilikuwa linasisitiza kuwa suala la eneo la Jerusalem ni suala linalotakiwa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo kati ya Israel na Palestina na kwamba uamuzi wa Marekani haukuwa wa kisheria.

"Marekani haitaambiwa na nchi yoyote mahali pa kuuweka ubalozi wake" alisema Nikki Haley balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa.

"Tulichoshuhudia leo kwenye baraza la usalama ni matusi. Haitasahaulika," alisema Haley aliyetaja hatua hizo kama kwa mara nyingine umoja wa mataifa umeonesha kutokujali katika kutatua kwa nia nzuri mzozo wa Israel na Palestina.