Pata taarifa kuu
CHILE-UCHAGUZI

Rais wa zamani wa Chile Pinera aongoza kwenye uchaguzi wa duru ya pili

Bilionea na Rais wa zamani wa Chile Sebastian Pinera anaonekana kuongoza katika uchaguzi wa duru ya pili dhidi ya mpinzani wake wa karibu Alejandro Guillier.

El candidado presidencial Sebastián Piñera da un discurso tras liderar la primera vuelta de las elecciones el 19 de noviembre de 2017 en Santiago de Chile.
El candidado presidencial Sebastián Piñera da un discurso tras liderar la primera vuelta de las elecciones el 19 de noviembre de 2017 en Santiago de Chile. Fuente: Reuters.
Matangazo ya kibiashara

Huku karibu asilimia 82 ya kura zote zikiwa zimehesabiwa mpaka kufikia usiku wa kuamkia leo, tume ya uchaguzi imesema Pinera amepata asilimia 54.1 ya kura zote dhidi ya mpinzani wake aliyepata asilimia 45.49.

Tangazo la matokeo haya ya awali liliamsha shamrashamra kwenye makao makuu ya kampeni ya Pinera mjini Santiago pamoja na viunga vingine vya nchi hiyo.

Uchaguzi huu ulilazimika kwenda kwenye duru ya pili baada ya Pinera aliyeongoza nchi hiyo katika ya mwaka 2010 hadi 2014 kupata asilimia 36.6 ya kura zote huku Guillier aliyeshika nafasi ya pili akipata asilimia 22.7.

hata hivyo zaidi ya raia milioni 6 waliojiandikisha kama wapiga kura hawakushiriki kwenye uchaguzi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.