Pata taarifa kuu
ARGENTINA-AJALI-USALAMA

Zoezi la kutafuta nyambizi iliyopotea lasitishwa Argentina

Nchini Argentina, jeshi la wanamaji lilitangaza siku ya Alhamisi Novemba 30 kuwa halina matumaini ya kuwapata wakiwa hai wafanyakazi 44 wa nyambizi San Juan iliyotoweka katika pwani ya Patagonia tangu Novemba 15.

Afisa wa jeshi la wanamaji la Marekani akiwa katikandege ya inayoshiriki zaoezi la kutafuta nyambizi San Juan iliyotoweka kusini mwa bahari ya Atlantic, Novemba 26, 2017.
Afisa wa jeshi la wanamaji la Marekani akiwa katikandege ya inayoshiriki zaoezi la kutafuta nyambizi San Juan iliyotoweka kusini mwa bahari ya Atlantic, Novemba 26, 2017. Argentine Navy
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kutafuta nyambizi hiyo linaendelea, lakini operesheni ya kuwapata wakiwa hai wafanyakazi 44 wa nyambizi hiyo imemalizika. Uamuzi huo ulitangazwa na msemaji wa jeshi la wanamaji la Argentina siku ya Alhamisi usiku, siku kumi na tano baada ya kutoweka kwa manowari San Juan. Hakuna matumaini ya kuwapata hai wafanyakazi hao, mmoja wa maafisa wa jeshi wanashiriki zoezi hilo amesema.

Familia nane za wafanyakazi 44 wa manowari San Juan zimebaini kwamba zitafungua mashtaka. Wanahisi kuwa ndugu zao walitumiwa kwa kuuawa. Ni kweli kuwa jeshi la wanamaji la Argentina lilificha taarifa muhimu kwa siku kadhaa, kama ripoti ya mwisho ya kamanda wa nyambizi hiyo, akibaini kutokea kwa hitilafu ya betri na moto kutokea muda mchache baadae.

Nyambizi hiyo ya San Juan ilikumbwa na mkasa huo ilipokuwa ikirejea kutoka katika shughuli zake za kawaida keneo la Ushuaia.

Ikiwa hakuna matumaini kwa familia ya wafanyakazi wa nyambizi ya San Juan, mamlaka bado inatarajia kupata nyambizi hiyo, au mabaki yake. Ndege na meli kutoka nchi kumi na nane zinashiriki katika zoezi la kutafuta manowari hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.