Pata taarifa kuu
COLOMBIA-ELN-USALAMA

Waasi wa ELN: Tuko tayari kusitisha mapigano hadi Januari 2018

Wakati ambapo mkataba wa kusitisha mapigano kati ya serikali ya Colombia na kundi la waasi la ELN uko hatarini, waasi wa ELN wametangaza kwamba wako tayari kuheshimu mkataba huo hadi Januari 9, kama walivyokubaliana na serikali, amehakikisha kiongozi wa mazungumzo wa kundi hilo mjini Quito.

Pablo Beltran, mkuu wa mazungumzo kwa upande wa waasi wa Colombia wa ELN, Novemba 7, 2017 Sangolqui, Ecuador.
Pablo Beltran, mkuu wa mazungumzo kwa upande wa waasi wa Colombia wa ELN, Novemba 7, 2017 Sangolqui, Ecuador. AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano maalum na shirika la habari la AFP, Pablo Beltran, kiongozi wa kundi la waasi la ELN, amekosoa serikali kutotimiza majukumu yake kwa mashambulizi dhidi ya viongozi wa jamii na watetezi wa haki za binadamu, ambapo 200 miongoni mwao wameuawa tangu mwezi Januari 2016, kwa mujibu shirika moja la haki za binadamu nchini Colombia.

Alitaja mauaji yaliyotekelezwa na waasi wa kiongozi mmoja anayeunga mkonoserikali, wakati ambapo makubaliano ya kusitisha mapigano ulikua ukiendelea kutekelezwa tangu Oktoba 1, na amekataa kuwa waasi wa ELN, wamegawanyika.

Katika kijiji cha kifahari cha Hacienda, mjini Quito, ambapo kunazungumziwa makubaliano kama yale yaliyoafikiwa mwaka 2016 na waasi wa kundi la FARC, Bw Beltran amesema kuwa serikali haiheshimu makubaliano iliyoafikiana na kundi hilo la zamani ambalo lilibadili na kuwa chama cha kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.