Pata taarifa kuu
MAREKANi-UGAIDI-USALAMA

Trump amwita mshambuliaji wa New York mgonjwa wa akili

Rais wa Marekani Donald Trump ameshutumu shambulio la kigaidi ambalo limeua watu nane katika jiji la New York na kusema ni kitendo cha wazimu.

Wachunguzi wakiwa kwenye eneo la shambulio. Hii ni mara ya kwanza tangu Septemba 11, 2001 shambulio kugharimu maisha ya watu mjini New York.
Wachunguzi wakiwa kwenye eneo la shambulio. Hii ni mara ya kwanza tangu Septemba 11, 2001 shambulio kugharimu maisha ya watu mjini New York. ©REUTERS/Brendan McDermid
Matangazo ya kibiashara

Akiandika katika ukurasa wake wa Twitter rais Trump amesema shambulio hilo katika jiji la New York linaonekana kutekelezwa na mtu mgonjwa sana na mwenye wazimu na kuongeza kwamba,Utekelezaji wa sheria unafuata hivi kwa karibu.

Ripoti za mapema za mashuhuda zinaonyesha kwamba mshambuliaji alijirusha kwa wapanda baiskeli na watembea kwa miguu huko Lower Manhattan na kupaza sauti akisema "Allahu akbar"yaani "Mungu ni mkuu" kabla ya kupigwa risasi na polisi.

Hili ni tukio la kwanza la kigaidi tangu rais Trump aingie madarakani, ingawa kumekuwa na mashambulizi kadhaa ya risasi na mauaji ya kisiasa.

Trump aliingia madarakani akiapa kupambana na kile alichoitwa ugaidi mkubwa wa Kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.