Pata taarifa kuu
MAREKANi-UNESCO-USHIRIKIANO

Marekani yatangaza kujiondoa katika Unesco

Marekani imetangaza Alhamisi hii (Oktoba 12) kuwa imejiondoa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), ikishutumu taasisi kufanya "ubaguzi dhidi ya Israel".

Makao makuu ya Unesco mjini Paris.
Makao makuu ya Unesco mjini Paris. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova, ametangaza Alhamisi hii Oktoba 12 kuwa alipewa taarifa na Waziri wa Mashauriano ya Kigeni, Rex Tillerson, uamuzi wa Marekani wa kujiondoa katika Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni, akishutumu taasisi hiyo kuwa "inapinga Israeli".

Katika taarifa yake, Irina Bokova amesema "anasikitishwa sana" na uamuzi huo. "Utu ni muhimu kwa majukumu ya Unesco kwa kutunza amani na usalama wa kimataifa dhidi ya chuki na vurugu kupitia ulinzi wa haki za binadamu na heshima ya binadamu" Irina Bova amesema.

Marekani iliwahi kujiondoa kwenye Unesco kati ya mwaka 1984 na mwaka 2003. Marekani ambayo ni mshirika wa karibu wa Israeli, iliwahi kusitisha mchango wake wa kifedha kwa Unesco, yenye makao yake mjini Paris, mnamo mwaka 2011 kufuatia kukubaliwa kwa Palestina. Sera ya Marekani ni kupinga utaratibu wowote wa kuitambua Palestina kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa mpaka pale mkataba wa amani utakua umepatikana Mashariki ya Kati.

Marekani inatishia kutekeleza uamuzi wake

Mapema mwezi Julai, Marekani ilionya kurejelea uhusiano wake na Unesco, na kuuita "ukiukwaji wa historia" uamuzi wake wa kutangaza mji wa kale wa Hebron katika Ukingo wa Magharibi, "eneo linalolindwa" la urithi wa dunia. Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, amesema kuwa mpango huu "unaharibu sifa la shirika la Umoja wa Mataifa ".

Hebron ina wakazi 200,000 Wapalestina na baadhi ya mamia ya walowezi wa Israel ambao wamejificha eneo linalolindwakeshi la Israel karibu na eneo takatifu ambalo Wayahudi wanaloliitwa kwa jina la kaburi jina la mababu na Waislamu, Msikiti wa Ibrahim. Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu wakati huo alielezea uamuzi wa Unesco kama "udanganyifu". Miezi michache kabla, Unesco iliitambua Israeli kama kikosi kinachokalia Jrusalemu kinyume na sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.