Pata taarifa kuu

Korea kaskazini, Chad na Venezuela zaongezwa kwenye marufuku ya kuingia Marekani

Serikali ya Marekani imeziongeza nchi za Korea kaskazini, Venezuala na Tchad katika orodha ya nchi ambazo raia wake wanazuiwa kuingia nchini humo kwa sababu za kiusalam.

Marufuku ya kuingia nchini Marekani sasa inahusu kwa taifa lolote ambalo halijaanzisha uhusiano wenye nia njema na mtu au taasisi ya Marekani.
Marufuku ya kuingia nchini Marekani sasa inahusu kwa taifa lolote ambalo halijaanzisha uhusiano wenye nia njema na mtu au taasisi ya Marekani. REUTERS/James Lawler Duggan
Matangazo ya kibiashara

Sudani ambayo ni miongoni mwa nchi sita za kiislam zilizokuwa katika orodha hiyo imeondolewa, huku idadi ya nchi hizo ikifikia nchi nane, ikiwa ni Iran, Libya, Syria, Somalia na Yemen.

Vikwazo hivyo vinatotiana kutoka nchi hadi nyingine. Wananchi wote wa Korea ya Kaskazini na Tchad wanazuiliwa kuingia nchini Marekani, wakati nchini Venezuela vikwazo hivyo vikiwakumba wajumbe wa serikali na familia zao.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Tweeter Donald Trump amesema usalama wa marekani ndio kipao mbele chake, na kwamba hawawezi kukpokea nchini Marekani kile ambacho hawawezi kudhibiti.

Kwa mujibu wa amri hiyo iliyosainiwa na rais Donald Trump, idadi ndogo ya nchi kati ya makadirio ya nchi 200 bado hazijabadilika katika masuala ya usimamizi wa utambulisho na ushirikiano katika kubadilisha taarifa. Katika hali nyingine, nchi hizo pia zina uwepo mkubwa wa Ugaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.