Pata taarifa kuu
MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO

Marekani kufunga ubalozi wake Cuba

Marekani kupitia Waziri wake wa Mashauriano ya Kigeni Rex Tillerson imesema inathamini uwezekano wa kufunga ubalozi wake nchini Cuba,. Kauli hii inakuaja baada ya kutokea mlolongo wa mashambulizi ya kelele kwa wafanyakazi wa Marekani nchini Cuba.

Marekani inatathmini kufunga ubalozi wake Cuba.
Marekani inatathmini kufunga ubalozi wake Cuba. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Marekani imeiambia Cuba kuwa ina jukumu la kuwalinda wafanyakazi wote wakigeni wakiwemo.

Zaidi ya wafanyakazi 20 wa ubalozi wa Marekani wanakabiliwa na matatizo ya kupoteza uwezo wa kusikia au kupatwa na mfadhaiko kutokana na kauli hiyo.

Mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana rais wa Marekani, Donald Trump, alitishia kufutilia mbali sera ya rais Barack Obama ya kurejesha uhusiano kati ya Marekani na Cuba wakati atakapochukua madaraka Januari mwakani huu.

Trump alisema uamuzi huo utategemea utawala wa kikomunisti mjini Havana, kuweka sera ambazo zitaimarisha hali ya maisha kwa raia wa nchi hiyo, na wale waliochukua uraia wa Marekani na wale wa Marekani.

Utawala wa rais Obama umejitahidi kurejesha uhusiano na utawala wa Havana, baada ya uhasama uliodumu kwa zaidi ya miaka hamsini.

Wakati huo Trump alimtaja hayati Castro kama kiongozi mkatili wa kiimla ambaye aliwakandamiza raia wake kwa miongo kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.