rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Majanga ya Asili Cuba Marekani

Imechapishwa • Imehaririwa

Kimbunga Irma chafanya uharibifu Cuba baada ya visiwa vya Carribean

media
Picha ya Satellite ya Kimbunga Irma nchini Cuba, Septemba 8, 2017. Courtesy NASA/Handout via REUTERS

Kimbunga Irma kimesababisha maporomoko nchini Cuba baada ya kupiga eneo hilo kikiwa na nguvu ya kiwango cha juu daraja la tano usiku wa Ijumaa, watabiri wa Marekani wamesema, baada ya kusababisha maafa na uharibifu katika visiwa vya Caribbean.


Kimbunga hicho kinaelezwa kuwa na upepo mkali wa kilomita 260 kwa saa na kilikuwa kikielekea magharibi kwa mwendo wa kilomita 20 kwa saa, na kusababisha tishio kubwa kwa jimbo la Florida nchini Marekani.

Gavana Rick Scott aliiambia CNN kuwa “watu wanapaswa kuelewa, ikiwa uko katika eneo la uokoaji, unapaswa kuwa mwangalifu sana, unapaswa kuondoka sasa,kwa kuwa dhoruba hii ni kali zaidi kuliko taifa letu”.