Pata taarifa kuu
HAITI-MAREKANI-TABIA NCHI

Kimbunga Irma kupiga Haiti, Cuba na maeneo mengine

Kimbunga Irma kinaendelea na uharibifu wake kikielekea katika Jamhuri ya Dominika na Haiti. Mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince na nchi nzima viko katika tahadhari nyekundu, lakini pwani ya kaskazini iko katika hatari zaidi.

Kimbunga Irma kinatarajiwa kupiga nchini Hati.
Kimbunga Irma kinatarajiwa kupiga nchini Hati. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, kimbinga Irma kinatarajiwakupiga pwani ya kaskazini mashariki ya Cuba kabla ya kufikia kusini mwa Florida siku ya Jumapili alasiri.

Irma sasa iko mbele ya pwani ya Jamhuri ya Dominika na inatarajiwa kupiga nchini Haiti usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi. Nchi hii bado iko katika tahadhari nyekundu. Ingawa kimbunga hiki hakitapiga zaidi nchini Haiti, mvua kumbwa na upepo mkali vinatarajiwa, labda kiwango chake kitakua kidogo kuliko iinavyotarajiwa.

Kimbunga Irma limesababisha uharibifu mkubwa katika visiwa vya Caribbean na kuwaua takriban watu 14.

Kuna wasi wasi kuwa ugonjwa unaweza kusambaa kwa haraka maeneo ambapo maji ya kunywa na huduma za usafi zimeathirika, na maafisa wameonya kuwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka.

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Care France, aliyehojiwa na RFI, amewataka wakazi wa pwani "kusikiliza maelekezo ya viongozi wa maeneo hayo, watii na waondoke maeneo hayo". Mapendekezo mengine ni "kuweka chakula na kuhakikisha kuwa wana chakuala cha kutosha kwa siku chache zijazo".

Haiti, Cuba na visiwa vya Turks na Caicos vinajiandaa kwa kuwasili kwa kimbunga Irma, ambacho tayari kimefanya uharibu mkubwa katika visiwa vingine vya Caribbean.

Mawimbi makubwa, mafuriko na upepo mkali vinatarajiwa huku maafisa wa serikali ya Haiti wakizunguka kila nyumba kushawishi watu waondoke.

Nchini Cuba, mamia na maelfu ya wananchi wameambiwa waondoke majumbani mwao.

Cuba ni kisiwa kikubwa katika eneo la Caribbean ,ambacho kipo katika mkondo wa kimbunga.

Kimbunga Irma tayari kimefanya uharibifu mkubwa Barbuda, St Martin na visiwa vya Marekani vya Virgin, ambapo msemaji wa serikali amethibitisha watu wanne wamepoteza maisha.

Wakati huo huo, zaidi ya watu nusu milioni wameamriwa waondoke majumbani mwao katika jimbo la Florida kabla kimbunga Irma hakijapiga jimbo hilo la Marekani siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.