Pata taarifa kuu
Colombia-PAPA FRANCIS-AMANI

Papa kuzungumzia amani na wananchi wa Colombia

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis anatarajia kukutana Alhamisi hii mjini Bogota na rais Juan Manuel Santos, kisha na vijana na umati wa waumini katika misa ya kwanza ya ziara yake nchini Colombia, inayolenga amani baada ya miaka zaidi ya hamsini ya vita.

Katika ziara yake ya siku tano nchini Colombia, Papa Francis anatarajiwa kugusia mazungumzo ya amani yaliyofikiwa mwaka jana kati ya serikali na kikosi cha waasi cha Farc.
Katika ziara yake ya siku tano nchini Colombia, Papa Francis anatarajiwa kugusia mazungumzo ya amani yaliyofikiwa mwaka jana kati ya serikali na kikosi cha waasi cha Farc. REUTERS/Alessandro Bianchi
Matangazo ya kibiashara

Papa Francis atakutana leo mchana na rais wa nchi ya Colombia Juan Manuel Santos aliyetunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2016. Kisha atahutubia vijana katika eneo la Bolivar, katikati mwa mji wa Bogota, kabla ya misa katika eneo kubwa la mji mkuu wa Colombia.

Karibu watu 660,000 wanatarajiwa Alhamisi hii alasiri katika eneo la Bolivar, Magharibi mwa Bogota, kwa ajili ya moja kati ya misa nne ambazo Papa Francis ataongoza nchini kote.

Papa Francis anatarajiwa kuwasili mji mkuu wa Colombia, Bogota saa chache kutoka hivi sasa, ikiwa ni ziara ya kwanza kufanywa na Papa nchini humo ndani ya miongo mitatu.

Katika ziara yake ya siku tano, anatarajiwa kugusia mazungumzo ya amani yaliyofikiwa mwaka jana kati ya serikali na kikosi cha waasi cha Farc.

Ziara hii inakuja wakati ambapo waasi wa ELN ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo, wamekubali kuweka silaha chini kwa muda na kufanya mazungumzo ya amani.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos amekaribisha uamuzi huo wa kundi la waasi la ELN na kuita tukio hilo la miujiza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.