Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini yasema imefanikiwa kujaribu silaha ya Nyuklia

Korea Kaskazini inasema imefanikiwa kujaribu silaha ya nyuklia inayokwenda masafa ya mbali.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akionekana mwenye furaha baada ya jaribio la silaha za nyuklia Septemba 3 2017
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akionekana mwenye furaha baada ya jaribio la silaha za nyuklia Septemba 3 2017 REUTERS/Toru Hanai
Matangazo ya kibiashara

Pyongyang inasema hili ni jaribio lake la sita la nyuklia ambalo limefanikiwa katika siku za hivi karibuni.

Ripoti kutoka Korea Kaskazini zinasema silaha iliyojaribiwa ni bomu aina ya hydrogen yenye nguvu na uwezo kuzidi bomu ya atomic.

Wachambuzi wa mambo wanasema madai ya Korea Kaskazini yanastahili kuchunguzwa kwa makini huku wakisisitiza kuwa nchi hiyo ina uwezi wa kuwa na silaha hatari za nyuklia.

Tangu Septemba mwaka uliopita, Korea Kaskazini imekuwa ikifanya majaribo ya silaha zake licha ya kuwekewa vikwazo na Baraza la Umoja wa Mataifa.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon Un akiwa na maafisa wengine wa serikali wakikagua  mitambo ya nyuklia Septemba 3 2017
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon Un akiwa na maafisa wengine wa serikali wakikagua mitambo ya nyuklia Septemba 3 2017 KCNA via REUTERS

Umoja wa Mataifa na mataifa jirani kama China, Japan na Korea Kusini yameendelea kulaani majaribio haya na kusema ni hatari kwa usalama wa dunia.

Pyongyang inayojihami kwa silaha za nyuklia, kwa muda mrefu imetafuta njia za kufikisha mabomu ya atomic kwa Marekani, ambayo ni adui yake mkubwa.

Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe amesema kuwa jaribio la sita la nyuklia la Pyongyang "halikubaliki kabisa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.