Pata taarifa kuu
MAREAKNI-URUSI-USHIRIKIANO

Marekani yaamuru kufungwa kwa ubalozi wa Urusi San Francisco

Marekani iliamuru kufungwa kwa ubalozi mdogo wa Urusi katika jimbo la San Francisco, pamoja na ofisi mbili za kidiplomasia katika miji ya Washington na New York. Tangazo hili linakuja siku moja kabla ya kuanza kutekelezwa vikwazo kwa wafanyakazi katika baloxi za Marekani nchini Urusi.

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesikitishwa na kuengezeka kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili.

Marekani iliitaka Urusi hadi Septemba 2 kuwa imefunga ubalozi wake mdogo katika jimbo la San Francisco na ofisi mbili katika miji ya Washington na New York katika kukabiliana na kupungua kwa kasi kwa wafanyakazi wa balozi za Marekani nchini Urusi.

Balozi mpya wa Urusi mjini Washington alianza kuhudumu siku ya Alhamisi. Anatoli Antonov amekosolewa kuwa na sifa mbaya.

Shutuma za Urusi kuingilia katika kampeni za uchaguzi za Marekani ambazozinachukuliwa kwa umakini sana na Wamarekani, na hata kama rais mwenyewe anataka kutuliza hali hiyo, Bunge la Congress na serikali wameendelea kuonyesha msimamo wao dhidi ya Urusi.

Serikali ya Urusi ilitwataka wafanyakazi 755 wa balozi za Marekani nchini Urusi kuondoka nchini humo hadi Septemba 1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.