Pata taarifa kuu
VENEZUELA-USALAMA

Wafuasi wa Maduro kuandamana dhidi ya Marekani kuingilia masuala ya Venezuela

Nchini Venezuela, wafuasi wa rais wa Venezuela Nicolas Maduro wanaendelea kuandamana dhidi ya rais wa Marekani Donald Trump na vitisho vyake vya kuingilia kijeshi nchini humo. Rais Nicolas Maduro, tayari amendaa mazoezi ya kijeshi ya ulinzi.

Nchini Venezuela, maelfu ya wafuasi wa rais Maduro waliandamana Agosti 14, 2017dhidi ya vitisho vya Marekani kuingilia kijeshi nchini humo.
Nchini Venezuela, maelfu ya wafuasi wa rais Maduro waliandamana Agosti 14, 2017dhidi ya vitisho vya Marekani kuingilia kijeshi nchini humo. AFP/Ronaldo Schemidt
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu Agosti 14, maelfu ya wafuasi wa rais Nicolas Maduro, wakivalia shati nyekundu, waliandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo, huku wakiimba nyimbo zinazompinga rais wa Marekani Donald Trump.

Maandamano haya dhidi ya Donald Trump yaliandaliwa kwa minajili ya kupinga vitisho vya Marekani vya kuingilia kijeshi nchini humo. Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameagiza vikosi vya jeshi kujiandaa kwa hali yoyote inayoweza kutokea.

"Nimetoa agizo kwa uongozi wa majeshi kuanzisha mazoezi ya kiraia na kijeshi katika ngazi ya kitaifa kwa ajili ya ulinzi wa jeshi la Venezuela, mazoezi ambayo yatafanyika tarehe 26 na 27 Agosti nchini kote" , rais Maduro amesema.

Wakati huo huo viongozi wa upinzani wanaochukuliwa na rais Maduro kama wasaliti, wameendelea kushikilia msimamo wao na kusema kuwa wanakaribisha hatua ya Marekani.

Rais ameagiza tume ya ukweli ya Bunge jipya la Katiba kufungua kesi dhidi viongozi hao wa upinzani. watashitakiwa kuwa waliomba Marekani kuingilia kati nchini Venezuela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.